Friday, March 27, 2009

Namna ya Kubusu

Namna ya Kubusu


-Sogeza midomo yako kama ilivyo (umeifumba lakini iko-relaxed) kwenye midomo ya unaetaka kumbusu…..kisha itulize midomo hiyo juu yake na sasa toa “busu kavu” juu ya midomo yake kisha jitoe alafu rudi tena x3…..1)

-inua uso wake kwa kutumia kidole (hii ni kwa wanaume) na mbusu moja kwa moja kwa kugusanisha pua kiaina…2)

-Busu kwa kupindisha shingo/kichwa ili kutogusanisha pua zenu…3)

-ukiwa umepindisha kichwa/shingo…mshike mkono au mkumbatie kiasi na busu tena.


Ukiona/hisi anajisogeza au anakupa ishara kuwa uendelee kwa kufungua mdomo kiaina, kukushika mkono/kifua/kitambi/kiuno au kuweka mkono kwenye bega basi endelea na “busu nyevu” kwa kubusu ktk mtindo wa kulamba-kunyonya mdomo(lips) wa chini na tulia hapo kwa sekunde chache kisha pokea ulimi wake kwa ulimi wako (bila kuachama…ni mumo kwa mumo)alafu ukwepe na kisha rudi kwenye midomo na busu lip ya juu…..


Ongeza ujuzi wako sasa…na kumbuka kupumua kwa kutumia pua sio unampumulia mwenzio mdomoni….(atashiba hewa) au unabada pumzi. Unaweza kufumba macho au kukodoa....inategema na wakati wenyewe.


Kuna aina tofauti za kubusu ili kutuma ujumbe kwa mpenzi wako lakini busu zote zinahusisha ulimi na mate. Unaweza ukapewa busu wewe ukadhani ni kawaida (kama hujui) lakini mwenzio anakwambia
-amechoka,
-anakupenda,
-anashukuru,
-amefurahi kukuona,
-hataki kungonoana siku/wakati huo,
-hana raha/hujamfurahisha,
-anataka kuwa peke yake,
-ana machungu,
-yuko busy n.k.


Busu la Kifaransa a.k.a denda


Unatakiwa kuwa “kissable” kwa kuwa na midomo laini na isiyo na mipasuko au ngozi-ngozi, hakikisha kinywa chako ni kisafi hasa ulimi, hakikisha unakunywa maji au kinywaji chochote kitakachosaidia kuondoa ukavu wa mdomo wako, vilevile jifunza kuongea na kucheka mara kwa mara ili domo lisichache/vunda.


Safisha kinywa ikiwa umekula chakula chenye shombo na epuka kula vyakula vyenye vitunguu swaumu pia kwa wavutaji sigara harufu yake mdomoni hunuka kama mavi akyanani…..kama ni mvutaji basi safisha kinywa au kula kitu kichachu na kitamu kama chungwa, embe, nanasi au unaweza kujaribu mvinyo (wine).

Unatakiwa kuwa na uhakika mwenzi yuko tayari kubusiwa sio unakurubuka na kufungua mdomo wa mwenzio na ulimi, unatakiwa kwenda hatua-kwa hatua...


Ukiona kuwa mwenzio yuko tayari basi ndio unapaswa kuendelea na busu ya mate/ulimi. Ninaposema mate sina maana upeleke kimiminika chako mdomoni mwa mwenzio la hasha! Pia ninaposema ulimi sio kwamba uzunguushe ulimi wako kwenye fidhi za meno yake na kuupeleka ulimi mpaka kooni…..utamtapisha mwenzio.


Busu sio tiketi/tikiti ya kufanya ngono japo kuwa ukaribu wenu unaweza kuwafanya mhisi kuwa mnataka/tamani kuendelea na hatua nyingine yakuingiziana mikono chupini na kushikana mazingira yenu nyeti, na badala yake kumbatia busu na enjoy the moment ...

Natambua wazi kuwa kuna watu wengi hawajui kubusu kwa kutumia ulimi a.k.a busu la Kifaransa na kuhakikishia hata baadhi ya wafaransa hawajui kucheza na ndimi zao...hivyo hauko peke yako.

No comments:

Post a Comment